KCB wajizatiti na msimu mpya wa ligi Kenya
Klabu ya KCB imekamilisha usajili wa wachezaji wapya 13 kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kuingia mkataba wa miaka miwili na kocha Frank Ouna ili kukiendesha kikosi katika msimu mpya wa ligi nchini kenya .
Ouna alishawahi kuwa kocha wa timu ya Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenta Harambee Stars .
Mkurugenzi wa rasilimali wa KCB Group na msimamizi wa klabu Paul Russo amesema kuwa mabadiliko yote yanatoka na lengo la kuifanya timu ya The Bankers kuwa timu bora katika msimu mpya wa ligi kuu nchini Kenya unaoanza mwaka huu
KBC imewanunua Tubana Jemus na Mugabo Gabriel wa Rwanda, mshambuliaji wa Burundi Hemedy Murubose na kipa Jamal Manyika na mshambuliaji Jamal Mwalumbeko kutoka Tanzania.
Klabu hiyo imefanya pia usajili wa wachezaji wa ndani wakiwemo Joseph Okath wa Bandari,Badi Baraka na kiungo Michael Mutinda wa Thika United,kiungo wa Kati Bernard mangoli ,Eston Esiye wa kakamega, kiungo wa kati wa Black Stars Nichodemus Onyango, Clinton Kisiabuki wa Nakumats FC na mshambuliaji wa Ushuru Benson Amiada
Bankers pia wamefanikisha kuupata uwanja wa Machakos uliopo Naivasha kuwa uwanja wao wa nyumbani katika michezo ya msimu wa 2018/2019.
Benchi la ufundi la klabu hiyo litaundwa na kocha mkuu Frank Ouna ,kocha msaidizi Elvis Ayany pamoja na Ezekiel Akwana aliyezifua AFC leopards and Nakuru All Stars .
mkufunzi Mwenye miaka 36 Michael Oyando na kocha wa magoli kipa Alex Mwangi.Nae Marcel Oile atajiunga kama kocha wa nguvu wakati Collins Kiama akiwa physiotherapist wa klabu hiyo.
Usimamizi wa timu hiyo utajumuisha Paul Russo kama msimamizi,mwenyekiti Azu Ogola makamu mwenyekiti Bramwell na Meneja wa klabu hiyo Okal Joseph.