Michelle Katsvairo atua Leopards
Mshambulizi wa Zamani wa timu ya Singida United Michelle Katsvairo anatarajiwa kujiunga na team ya AFC Leopards baada ya kumfurahisha kocha Nikola Kavazovic katika mechi ya majaribio.
Raia huyo wa Zimbabwe aliichezea Leopards siku ya Jumatano katika mechi ya kirafiki didhi ya timu la daraja la pili Wazito FC katika uga wa Camp Toyoyo mjini Nairobi. Mechi hiyo iliishia sare ya moja kwa moja.
Baada ya mechi hiyo, kocha mkuu wa Leopards Nikola Kavazovic alieleza kuridhika kwake na mchezo wa raia huyo wa Zimbabwe na akathibitisha kuwa mshambulizi huyo atajiunga na miamba hao wa Kenya.
“Mchezo wake umeniridhisha, atapewa Kandarasi. Ni mchezaji mzuri na nina imani kuwa ataisadia timu yangu,” alisema Nikola.
Katsvairo aliichezea Singida United mwaka uliopita akiwa kwenye mkopo kutoka kilabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Aliifungia Singida mabao matatu kabla ya kuigura mwezi wa Januari 2018 akidai kilabu hiyo ilikuwa imeshindwa kulipa mshahara wake.
Kufikia sasa Leopards imewasajili wachezaji watatu. Isaac Kipyegon amejiunga na Leopards kutoka Zoo FC na Joshua Mawira amerejea kwenye timu baada ya kuigura mwezi wa Januari. Raia wa Zambia Shadreck Chimanya pia amejiunga na timu. Kipa wa Rwanda Eric Ndayishimiye pia anatarajiwa kusaini baada ya Mazungumzo kukamilika.