Neymar na Mbappe hatihati kucheza Klabu Bingwa Ulaya
Washambuliaji wa klabu ya PSG Kylian Mbappe na Neymar huenda wakaikosa mechi dhidi ya Liverpool jumatano ya tarehe 28 Novemba kwenye michuano ya kutokana na majeraha walioyapata wakitumikia timu zao za taifa.
Mbappe amepata majeraha akiwa na timu yake ya taifa Ufaransa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Uruguay jana baada ya kuanguka na kuumia bega akiwa anajaribu kumkwepa kipa wa Uruguay Martin Campana dakika ya “36”. Kutokana na kuumia vibaya huweenda atakaa nje ya uwanja kwa mda mfupi.
Huku Neymar ameumia katika mechi ya kirafiki ya taifa lake la Brazil dhidi ya Cameroon hapo jana katika dakika ya 6 ya mchezo akiwa nataka kupiga krosi kuelekea lango la Cameroon na kuanguka chini kwa maumivu yaliosababisha kushidwa kumaliza mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Richarlison wa Everton.

Kwa mujibu wa Neymar na daktari wa timu ya Brazil wamesema sio tatizo kubwa la kufanya kukosa mchezo huwa dhidi ya Liverpool huku Mbappe haijulikani kama atakuwepo kwenye mechi hiyo.