Uefa Nations League imefanikiwa kuliko tulivyotarajia “ – Rais wa UEFA Aleksander Ceferin.
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA Aleksander Caferin amesema michuano mipya ya barani humo UEFA Nations League imeleta mafanikio makubwa tofauti na walivyotarajia hapo awali.
Michuano hiyo ilitengenezwa kwa ajili ya kuondoa mechi za kirafiki zisizokuwa na maana, mwanzoni ilikosolewa na watu wakidai kuwa michuano hiyo haina maana yoyote ile na haileweki.
England, Switzerland, Uholanzi na Ureno zimefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambapo mechi za nusu fainali zitachezwa mwezi Juni mwakani.
Croatia na Germany ni moja ya mataifa makubwa ambayo yameshuka daraja kutoka League A na kuingia League B baada ya kushika nafasi za mwisho katika makundi yao.
‘ Nations League imefanikiwa zaidi kuliko tulivyofikiria. Tumekuwa tukipata malalamiko kutoka mataifa ya makubwa ya mpira- “ Tunacheza na mataifa madogo, hatuchezi sisi kwa sisi (wakubwa) – na tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka mataifa madogo – “Sisi huwa hatushindi “, ‘. Rais wa UEFA Alesander Caferin alisema hivyo katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Brussels.
Michuano hiyo pia inatoa nafasi kwa timu kufuzu michuano ya Euro 2020.
Rais huyo amesema kupanda na kushuka daraja katika michuano hiyo imefanya iwe na mvuto zaidi, licha ya kuwa hajafurahi kuona timu yake, Slovenia ikishuka daraja kwenda League D wakitokea League C.
Andrea Agnelli, mwenyekiti wa Juventus aliwaambia pia waandishi kuwa michuano hiyo ya Nations League imekuwa ya mafanikio na anaamini wachezaji wameifurahia.