N’golo Kante kujitia kitanzi Chelsea
Kiungo wa klabu ya Chelsea N’golo Kante yupo tayari kusaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaofanya alipwe mshahara wa pauni 290,000 kwa wiki
Baada ya mazungumzo ya takribani miezi sita na klabu hiyo sasa wamefikia makubaliano na kumfanya kiungo huyo kuwa mchezaji anaelipwa zaidi Chelsea.
N’golo ambaye alikuwa mchezaji bora wa PFA katika msimu wake wa kwanza na klabu hiyo akitokea Leicester City akiwa bado ana mkataba wa miaka mitatu klabu hiyo imeona bado ana thamani kubwa na kuongeza mkataba wa miaka mitano.
Mfaransa huyo mwenye miaka 27 kwa mkataba wake wa sasa analipwa pauni 150,000 na klabu ya PSG ilikuwa tayari kumlipa mara mbili ya dau hilo , lakini dili limekwama baada ya chelsea kulifikia.
Kante ni moja ya wachezaji saba wa Chelsea walioanza katika mechi 12 za kwanza za msimu huu wa ligi kuu chini ya kocha Maurizio Sarri.