“Tia bidii zaidi“ Mwalala amsihi Hamisi
Kocha wa Bandari Bernard Mwalala amemsihi kiungo Abdalla Hamisi ajikakamue zaidi ili aweze kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Bandari.
Hamisi alijiunga na Bandari Juni kutoka kilabu ya Sony Sugar lakini imekuwa vigumu kwake kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Bandari.
Michael Luvutsi, Wilberforce Lugogo na Dan Guya ndio viungo ambao Mwalala amekuwa akiwatumia tangu alipoingia Bandari mwezi Juni kutoka Nzoia Sugar.
Kwenye mahojiano ya moja kwa moja, Mwalala alimsifia Hamisi ila akamsihi mchezaji huyo wa team ya Tanzania isiyozidi miaka 23 kutia juhudi zaidi.
“Hamisi ni mchezaji mzuri sana, pia bado ni mchanga kwa hivyo ana uwezo wa kuimarika zaidi. Kwa sasa hachezi kwa kuwa nina viungo wengi wazuri. Langu ni kumsihi aweke bidii zaidi ile aweze kupata nafasi ya kucheza. Ninataka apiganie nafasi yake kwenye timu kwa kutia bidii zaidi,” alisema Mwalala ambaye alikuwa mchezaji wa Yanga kitambo kabla kuifunza Coastal Union kama naibu Mkufunzi.
Bandari hivi sasa wako kwenye maandalizi ya msimu ujao utakao anza tarehe nane Disemba mwaka huu.