NEYMAR KUHUKUMIWA MIAKA 6 JELA
Nyota wa klabu ya PSG Neymar Jr anaweza akahukumiwa kifungo cha miaka 6 jela kutokana na tuhuma zinazomkabili za makosa ya kifedha katika usajili wake toka Santos kwenda Barcelona mwaka 2013.
Tuhuma hizi dhidi ya Neymar ziliibuliwa na kampuni la uwekezaji ya nchini Brazil waliolalamika kupata mgao mdogo toka kwenye uhamisho huo na kudai sehemu ya ada ya uhamisho ikifichwa na pande husika kinyume cha sheria.
Nchini Hispania hukumu ya kifungo chini ya miaka miwili hutolewa msamaha wa kutokwenda jela kwa kosa la mara ya kwanza hivyo Neymar kuwa katika hati hati ya kwenda jela kutokana na kosa lake kuwa na hukumu inayozidi miaka miwili.
Mzazi wa Neymar, Rais wa sasa wa Barcelona Josep Bartomeu Sandro Rosell—aliyekuwa rais wa Barcelona kabla ya kuachia madaraka mwaka 2014 baada ya kashfa hiyo kuzidi, na Santos wote wanashutumiwa kwa kosa hilo na pia wanatakiwa kufika mahakamani tarehe ya shitaka itakapotajwa.