Manchester City kuupanua uwanja wao
Klabu ya Manchester City ina mpango wa kuongeza ukubwa wa uwanja wao wa Etihad kufikia kuchukua mashabiki 63,000 na tayari wamekutana na mashabiki wao kuzungumzia suala hilo.
Kwa sasa uwanja huo una uwezo wa kuchukua mashabiki 55,097.
Klabu hiyo inatazamia kuongeza jukwaa la kaskazini ambapo zitakuwa zimeongezeka siti takribani 8,000.
Kampuni ya utengenezaji wa viwanja SGI hivi karibuni wamefanya mkutano wa mashabiki kwa niaba ya klabu wakijadili suala hiyo, ambapo imeelezwa ujenzi huo unatakiwa kuanza mwakani.
Klabu inayo shauku ya kuwashiriksha mashabiki ili kujua mapendeleo yao ya muonekano jukwaa hilo.
Inaelezwa kuwa maafisa wa klabu ya City wanafata kufata nyayo za klabu za Celtics na Borussia Dortmund kwa kutengeneza majukwaa ya kusimama yenye usalama.
Pia maafisa hao wa City wanataka kuhakikisha kuwa eneo kubwa la jukwaa hilo jipya liwe na bei nafuu zaidi kwa ajili ya mashabiki wa hali za kawaida.
Endapo ujenzi huu utaanza mwakani, utachukua muda wa miaka miwili, hivyo majukwaa hayo yatakuwa tayari kutumika kuanzia msimu wa 2021/22.