Christian Pulisic huyu hapa darajani
Klabu ya Chelsea imeonekana kushinda vita ya kuipata saini ya winga wa klabu ya Borussia Dortmund Christian Pulisic ambaye mkataba wake na timu hiyo ya Ujerumani unaisha mwaka 2020.
Mzaliwa huyo wa Marekani mkataba wake na Dortmund unafika kikomo mwaka 2020 na sasa Dortmund wameripotiwa kukubali kuweka pesa mfukoni kwa kumuuza mchezaji huyo mwisho wa msimu huu baada ya makubaliano ya mkataba mpya kushindikana.
Hata hivyo Chelsea wana haraka zaidi na kutaka dili hilo kukamilika mwezi Januari mwakani kutokana na kuwepo na tetesi za huenda wakafungiwa na FIFA kufanya usajili kwa kosa la kusajili wachezaji wa kigeni waliopo chini ya umri stahiki.
Pulisic,20, ni moja ya nyota wanaokuja kwa kasi katika ligi ya Bundesliga na amekuwa ni moja ya wanaongoza safu ya washambuliaji ya Dortmund msimu huu.
Mchezaji huyo ambaye amekuwa Dortmund tangu akiwa na umri wa miaka 16 awali ilitajwa kuwa atauzwa kwa kiasi cha takribani pauni milioni 70, lakini sasa inaonekana ada hiyo itashuka kuhofia kumpoteza bure mwaka 2020.