Valencia arusha dongo kwa Jose Mourinho.
Beki wa klabu ya Man United Antonio Valencia amefichua kuwa hapati nafasi ya kucheza kwenye klabu yake si kwa sababu ameumia kama anavyodai kocha wake Jose Mourinho.
Meneja wa Man United Jose Mourinho mwanzoni mwa mwezi huu alisema kuwa nahodha huyo ameumia na bado hayupo fiti kushuka dimbani
Lakini, akiwa katika majukumu ya timu ya Taifa ya Ecuador, beki huyo amedai kukosa dakika za kucheza si kwa sababu inavyodaiwa na kocha wake Jose Mourinho.
“ Kwa sasa nimekuwa sichezi , lakini ni maamuzi ya kimbinu zaidi “ Valencia aliiambia Area Deportiva ya nchini kwao
‘ Mchezaji ambaye yupo katika nafasi yangu (Young) amekuwa akicheza vizuri. Unatakiwa kuheshimu maamuzi.’
Valencia hajaichezea Man United tangu watoke sare na Valencia katika klabu bingwa Ulaya mwanzoni mwa mwezi Oktoba.
Mchezaji huyo mwezi uliopita aliingia kwenye uhasama kwa kuonekana kumkosoa Jose Mourinho baada ya ‘ku-like’ post ya Instagram ambayo iliandika kuwa kocha huyo anatakiwa kufukuzwa klabuni hapo.
Valencia amefunga goli la kwanza katika ushindi wa Ecuador wa 2-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Peru jana alhamisi usiku.