VAR yaingia ligi kuu nchini England
Klabu za ligi kuu nchini England zimekubaliana kuanza kutumia mfumo wa Video Assistant Referee (VAR) katika ligi hiyo.
Msimu wa 2019/20 ndio mfumo huo utaanza kutumika.
Katika kikao cha leo, vilabu vimepewa maendeleo ya majaribio ya VAR katika mechi za ligi hiyo msimu huu na kuongelea utumikaji wake katika michuano ya FA Cup, Carabao na ligi nyingine duniani, kila kitu kimejadiliwa kwa kina.
Hivyo baada ya makubaliano hayo, ligi hiyo sasa itatuma maombi rasmi kwenda kwa watengenezaji wa sheria za soka International Football Association Board (IFAB) na FIFA ili kuitumia VAR kuanzia msimu ujao.