Ronaldo aacha Toyota IST 6 mgahawani
Shilingi milioni 79 za Tanzania unaweza kununua Toyota IST 6 na chenchi ikabaki.
Ndani ya dakika 15 tu pesa hizo zilitumiwa na Cristiano Ronaldo katika mgahawa mmoja uliopo jijini London Jumatatu hii.
Ronaldo akiwa na mpenzi wake Georgina Rodriguez na rafiki zake wengine wawili wanaume waliingia katika mgahawa huo (Scott’s restaurant) na kuagiza chupa ya mvinyo ya Richebourg Grand Cru, huu ni mvinyo ghali zaidi duniani ukiuzwa kwa Pauni 18,000 ( Tsh Milioni 52.9) .
Mvinyo huo unaotoka mkoa wa Burgundy nchini France hupatikana kwa nadra sana na huwa haupo kwenye menu.
Baadae wakaagiza chupa ya mvinyo mwingine, 1982 Pomerol Petrus ambayo inauzwa pauni 9,000 ( Tsh Milioni 26.4) .
Inaripotiwa na vyombo vya habari vya Uingereza kuwa chupa hii ya pili hawakuimaliza.
Walikaa hapo kwa muda wa dakika 15 tu, ‘Bill’ ikaja ni pauni 27,000 ( Tsh Milion 79) , chanzo cha habari kinasema kuwa Ronaldo hakupepesa jicho, akalipa pesa hiyo na wakaondoka kwenda kuangalia michuano ya Tenesi ya ATP Finals inayoendelea katika jiji hilo la London.
Kitendo hicho katika mgahawa huo kiliongolewa usiku mzima , kilisema chanzo hicho