Benjamin Mendy arudi tena kitandani
Beki wa kushoto wa klabu ya Man City Benjamin Mendy amefanyiwa upasuaji katika goti lake la kushoto, lakini haijawekwa wazi ni muda gani atakuwa nje ya uwanja.
Mfaransa huyo alicheza dakika zote 90 katika mechi ya jumapili ambayo City waliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester United na jumatatu akaripoti katika kambi ya timu ya taifa ya France.
Jumatatu mchana akajitoa kwenye kikosi cha France na kusafiri mpaka Barcelona kufanyiwa uchunguzi ambapo ikagunduliwa anahitaji kufanyiwa upasuaji wa goti hilo.
Upasuaji wa beki huyo,24, umefanywa na daktari ambaye huwatibu wachezaji wa kocha Pep Guardiola Dr Ramon Cugat.
Daktari huyo pia ndiye aliyemfanyia upasuaj Mendy katika goti lake kulia msimu uliopita na kukosa mechi 43 za Man City.