Novak Djokovic afukuzia ubingwa wa ATP Finals
Mcheza tenesi namba moja kwa ubora duniani Novak Djokovic amefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya ATP Finals inayoendelea jijini London.
Djokovic amefika hatua hiyo baada ya kushinda kwa seti 6-4,6-1 dhidi Mjerumani Alex Zverev .
Djokovic,33, ambaye anafukuzia ubingwa wa ATP Finals wa kwanza tangu mwaka 2015 anakuwa ni mchezaji wa kwanza kufika hatua ya nusu fainali ya michuano hii.
“ Sifikirii ilikuwa ni tenesi ngumu lakini ushindi ni ushindi “ Alisema Djokovic
“ Sikutumikia sana lakini alifanya makosa yasiyo lazima mengi ambayo yamenisaidia kushinda. “
Zverev,21, mwenyewe baadae alisema uchovu pengine ni moja ya kilichochangia yeye kupoteza, akisema kuwa urefu wa msimu wa tenesi ni hatari.