Mourinho kasema Manchester City walikuwa na mechi mbili za kirafiki kabla ya kucheza nao
Usiku wa Jumapili ya tarehe 11 Novemba Manchester United walikuwa wageni wa Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza mzunguuko kwanza msimu wa 2018/2019, Manchester City walishinda mabao 3-1.
Mara baada ya kipigo hicho kwa Manchester United wengi walitamani kusikia kocha Jose Mourinho ambaye ana hulka ya majigambo ataongea nini sasa mbele ya waandishi wa habari? Atakuwa na jipya gani tena maana alivyo wafunga Juventus katika Ligi ya Mabingwa .
Jose Mourinho kama ilivyo kawaida yake hakosi cha kuongea, Mourinho amesmea Manchester City walikuwa na michezo miwili rahisi kabla ya kucheza na Manchester United, hivyo iliwasaidia kupata ushindi katika mchezo wa Derby tofauti na wao , Manchester City kabla ya mchezo wa derby alicheza na Southampton na Shakthar Donetsk.
Mourinho ameiambia BBC Radio 5 kuwa “Ni matokeo magumu sana kwa timu ambayo ilikuwa na mechi tatu ugenini ngumu ugenini ndani ya wiki moja, tena ikiwa na mchezo mgumu ugenini na timu kama Juventus halafu unacheza na timu ambayo ilikuwa na mechi mbili za kirafiki nyumbani dhidi ya Southampton na Shakhtar” Mourinho aliiambia BBC Radio 5