WAJUMBE WA FIFA WAAHIRISHA KIKAO CHA SULUHU KENYA
Mkutano uliyokuwa ufanyike kati ya wawakilishi wa shirikisho la soka duniani (FIFA) na shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) uliyokuwa ufanyike April 6 2020 umeahirishwa sababu ya corona.
Kikao hicho kilikuwa kikao ili kujadili mgogoro wa FKF uliyopelekea kushindwa kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa viongozi wa soka Kenya (FFK) uliyokuwa umepangwa kufanyika Machi 27 2020 kutokana na wizara ya michezo Kenya kuzuia.
Wajumbe wa FIFA wamethibitisha kuwa mkutano huo utafanyika tena Mei 2020 ili kutafuta suluhu iwapo tu hali itakuwa imerejea kama kawaida upande wa usalama wa kiafya kwa maana ya kuepuka mkusanyiko ambao ungeweza kuwa sababu ya kuenea kwa virusi vya corona.
Pamoja na kuahirisha huku barua iliyotumwa Kenya imeagiza kuwa kamati ya uchaguzi ipitie tena vigezo vya wagombea wa Urais, Makamu na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya FKF.