Deschamps kamrudisha Martial timu ya Taifa
Baada ya kuimarika kwa kiwango cha Anthony Martial katika mechi 7 kufunga magoli 7 akiwa na Manchester United, kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps ameshawishika kumuita Martial timu ya taifa tena baada ya kumuacha katika michuano ya Kombe Dunia 2018 nchini Urusi.
Martial sasa pamoja na kukosekana katika kikosi cha Ufaransa toka mwezi Machi mwaka huu, sasa anaungana na timu hiyo kwa ajili ya michezo miwili ya kimataifa, mchezo wa Nations League Novemba 16 dhidi ya Uholanzi ugenini na mchezo wa kirafiki dhidi ya Uruguay Novemba 20 2018.
Paul Pogba licha ya kuripotiwa kuwa majeruhi yaliopelekea kuukosa mmchezo wa Manchester United dhidi ya Manchester City, inaonekana atakuwa tayari kucheza michezo ya kimataifa baada ya kocha kumjumuisha kikosi hicho, hivyo inaaminika sasa Pogba yupo katika hali nzuri.