BURNLEY WAHOFIA KUFILISIKA
Mwenyekiti wa klabu ya Burnley Mike Garlick amesema timu yao itakuwa imefilisika kufiki mwezi wa nane kama msimu huu wa EPL hautakamilika na msimu ujao kuchelewa kuanza.
Garlick anasema watapoteza kiasi cha Pauni milioni 50 (Tsh Bilioni 141.9) kama msimu huu hautomalizika— na kuwaonya vilabu vingine kuwa watapoteza zaidi ya Pauni milioni 100.
“Ukweli ni kuwa, kama hatumalizi msimu na haipo wazi tarehe ya kuanza msimu ujao, sisi kama klabu tutakuwa hatuna hela kufikia Agosti. Huo ni ukweli.
“Siwezi kuongelea klabu zingine, sijui hali yao ya kifedha.
“Ninachoweza kuongea ni kwa klabu yetu na hali yetu” —— Garlick aliongea wakati akihojiwa na Sky Sports.
“Tulipiga kura kwa makubaliano kumaliza msimu, kwa hiyo ipo wazi kila mmoja anataka kumaliza kazi”
“Ni wazi kuwa kumaliza msimu kwa sasa ndio matokeo mazuri kwa klabu zote za EPL” – alimaliza Garlick