KOCHA WA HISPANIA AMKATAA NEYMAR
Kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Hispania Vicente del Basque ameeleza kutopendezwa na mbinu za mchezo ambazo hutumiwa na Neymar akiwa uwanjani.
Neymar amekuwa akipingwa na tabia yake ya kujiangusha na udanganyifu wa kufanyiwa madhambi na kuhesabiwa si vitendo vizuri vya kimichezo.
“Kwangu mimi (Neymar) si mfano mzuri wa kufuata,” —Del Bosque aliiambia Mundo Deportivo.
“Na kwa rekodi tu, ninaamini ni mchezaji mzuri.
“Ni wazi yupo katika tano bora yangu duniani. Lakini akiwa uwanjani anadanganya na kuigiza sana.”
Dunia ikiwa katika janga kubwa la virusi vya Corona, Del Bosque amesema kuwa inatakiwa liwe ni fundisho kwa kila mmoja.
Pia amesema kuwa msimu huu wa 2019/20 lazima umalizike.
“Ligi za ndani lazima zimalizike. Lazima wawepo mabingwa, wanaoshuka daraja,wanaopanda daraja, na vinginevyo.
“Msimu lazima ukamilike licha ya yote hayo” alisema Del Bosque