BAYERN MUNICH WAREJEA MAZOEZINI LEO JUMATATU
Klabu ya Bayern Munich imetangaza kurejea mazoezini leo April 06 kwa mara ya kwanza tangu Bundesliga isimamishwe Machi 13 kwa sababu ya virusi vya Corona.
Taarifa iliyoandikwa na Bayern Munich katika tovuti yao ilisomeka:
“Kikosi cha kwanza cha Bayern Munich kitarejea mazoezini katika kundi dogo kuanzia Jumatatu,April 6”
“Hii itafanywa katika kushirikiana na sera ya serikali na mamlaka husika”
Vinara hao wa Bundesliga wamesema mazoezi hayo yatafanya kibinafsi bila kuhusisha mashabiki.
“Ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona, Bayern inawataka mashabiki kuendelea kufuata maelekezo ya mamlaka na hivyo wasije katika uwanja wa mazoezi wa Bayern.” Waliongeza katika taarifa yao.
Mpaka sasa katika nchi ya Ujerumani zaidi ya watu 1,300 wamefariki kutokana na virusi vya Corona.
Tangu Machi 13 ligi ya Bundesliga iliposimamishwa, hakuna timu ilikutana kufanya kikao au mazoezi.
Tarehe ya Bundesliga kurejea bado haijawekwa wazi lakini awali ilitangazwa ligi hiyo kusimama mpaka April 30.