DE GEA ATOA MILIONI 700 HISPANIA
Si ndani ya uwanja tu, hata nje ya uwanja anaweza kuokoa. Kipa wa Manchester United David De gea ametoa msaada wa Pauni 270,000 (Tsh Milioni 755) katika mji wa Madrid ili kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona.
Staa huyo wa zamani wa Atletico Madrid imeelezwa hakutaja jina lake wakati amechangia pesa hiyo kwa mamlaka ya mtaa katika jiji la Madrid ili kusaidia vifaa vya matibabu na kusaidia familia zilizoathirika.
Lakini siri hiyo ilifichuliwa na Rais wa Jamii ya Madrid Isabel Diaz Ayuso alipoandika katika mtandao wake wa Twitter kumshukuru kwa mchango wake
Lakini siri hiyo ilifichuliwa na Rais wa Jamii ya Madrid Isabel Diaz Ayuso alipoandika katika mtandao wake wa Twitter kumshukuru kwa mchango wake.
“Ahsante De Gea. Msaada mkubwa ulioutoa kwa jamii ya Madrid utakuwa muhimu katika kupambana na COVID-19. Daima tunashukuru,tunajivunia wewe.” — aliandika Isabel
Mpaka jana Machi 26,2020 nchi ya Hispania kesi 57,786 za Corona zimeripotiwa, watu 7,015 wakipona na watu 4,365 wakiwa wamepoteza maisha