WACHEZAJI WA JUVENTUS WAKUBALI KUKATWA MISHAHARA
Baada ya vilabu vingi kuwa katika mvutano na wachezaji wao kwa kutaka kuwakata mishahara yao wakati huu mlipuko wa virusi vya corona, huku wachezaji wa Barcelona wakikataa makato ya asilimia 70.
Leo wachezaji wa Juventus kwa pamoja wameripotiwa kukubali kushiriki kuinusuru klabu yao isiyumbe kiuchumi kwa kukubaliana kukatwa mishara yao.
Wachezaji wa Juventus kwa pamoja wamekubali kukatwa huku Cristiano Ronaldo akikatwa pauni milioni 3.4 (Tsh Bilioni 9.7) jumla wachezaji wa Juventus watakuwa wameiokolea klabu yao euro milioni 90 (Tsh bilioni 231.4) kwa kukubali kukatwa mishahara yao katika kipindi hiki cha virusi vya corona.