AMISSI TAMBWE AKIRI KUIMISS VPL
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na Yanga SC Amissi Tambwe akiongea kwa njia ya simu na Azam TV mara baada ya hivi karibuni kuonekana jijini Dar es Salaam akiangalia Derby ya Simba na Yanga.
Leo ameeleza ni kitu gani anakumbuka katika soka la Tanzania hususani wakati akicheza Simba na Yanga SC, Tambwe aeleza kwa njia ya simu akitokea Burundi akieleza kuwa licha ya kuzoea pia alikuwa na ofa ya dola 100 za kimarekani kila akishinda.
”Kwanza ni sehemu ambayo nilikuwa nishazoea, ukiwa unachezea timu za Simba na Yanga ni timu kubwa sana Afrika kila mtu anajua, wakati nacheza Simba kwanza watu wengi walikuwa hawatarajii kama nitafanya vizuri kwa sababu niliingia kimya kimya sikuingia ile kwa kupambwa”
”Kwa hiyo watu wengi walikuwa wanajua kuwa sitofanya vizuri lakini Mungu alisaidiaga nikafanya vizuri, wakati nafika hapo kuna mwanachama mmoja wa Simba ni mkubwa hapo ni kiongozi alikuwa ananunua goli moja dola 100 ni kitu kilikuwa kinanipatia motisha sana”