DYBALA NA GIRLFRIEND WAKE WAUGUA CORONA
Nyota wa klabu ya Juventus ya nchini Italia Paulo Dybala pamoja ma mpenzi wake Oriana Sabatini wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Wote wawili wametengwa na kupatiwa matibabu licha ya kuelezwa kuwa hali zao ni nzuri, taarifa hizi zinakuja ikiwa ni siku chache zimepita toka azushiwe kupata virusi hivyo.
Hata hivyo licha ya kuwa wimbi la wachezaji wa Italia (Serie A) wanaoambukizwa virusi hivyo kuwa kubwa, Dybala anakuwa mchezaji wa tatu wa Juventus kupata maambukizi hayo baada ya Rugani na Matuidi.