NYOTA YA BRUNO FERNANDES YAZIDI KUNG’AA MAN UNITED
Kiungo mpya wa ManUnited rai wa Ureno Bruno Fernandes licha ya kuwa na muda mfupi toka aawasili Man United akitokea Ureno.
Fernandes ameendelea kung’aa akiwa ndio kwanza ana miezi miwili, Fernandes ametangazwa kwa mara ya pili mfululizo kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi wa klabu ya Man United.
Hata hivyo akiwa ndio kwanza amewasili Man United Januari 30 2020, Fernandes pia alikuwa mshindi wa tuzo za mchezaji bora wa klabu mwezi Februari , Mchezaji bora wa Ligi Kuu England wa mwezi na mchezaji bora wa EPL aliyechguliwa na mashabiki.