RAIS WA TFF KASEMA HAWATOPOKELEA VPL WACHEZAJI WALIOREJEA NCHINI KWAO
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amevipa onyo vilabu vya Ligi Kuu kuw huu sio wakati wa likizo kiasi cha kuwaruhusu wachezaji wao wa kimataifa warejee katika mataifa yao.
Karia ameeleza kupitia Azam TV kuwa Ligi imesimama kwa tahadhari ya virusi vya corona, hivyo wachezaji waliorejea kwenye nchi zao na kugoma kukaa nchini hawawezi wapokea wakirudi kwa sababu hawana uhakika kma watakuwa salama na virusi hivyo.
Hadi sasa mchezaji wa Simba SC raia wa Rwanda kwa mujibu wa picha za mitandao ya kijamii ni kuwa karejea kwao Rwanda wakati huu ambao serikali imesimamisha shughuli zote za kimichezo kwa siku 30 ili kuangalia hali ya mlipuko wa virusi hivyo.