“POMBE MI NAKUNYWA” —MKUDE
Kiungo wa klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania Jonas Mkude amekiri kuwa yeye ni mtumiaji wa pombe na hana sababu ya kukataa suala hilo.
Mkude amethibitisha hilo baada ya kuulizwa swali hilo leo katika mahojiano ya kipindi cha Sports HQ cha kituo cha Redio cha EFM
“Hakuna binadamu ambaye anakosa starehe, fikiria pia ninafanya starehe wakati gani?!
Sikatai, pombe ninakunywa. Ameshajua mama yangu mzazi,hata akijua mtu mwingine haisaidii.” -Alisema Mkude
“Pombe ninakunywa,lakini ninakunywa wakati gani?. Sijawahi kwenda mazoezini nikiwa nimekunywa “ alisisitiza Mkude