LALIGA YASIMAMISHWA KWA MUDA USIOJULIKANA
Viongozi wa soka wa Hispania wamesimamisha ligi ya soka nchini humo LaLiga kwa muda usiojulikana baada ya virusi vya Corona kuua zaidi ya watu 2000 nchini humo, ikiwa ni nchi ya pili kuathirika zaidi barani Ulaya nyuma ya Italia.
Shirikisho la soka nchini humo RFEF limetangaza pia ligi zote za nchi hiyo zitasimama mpaka pale serikali ya Hispania itakapotangaza hakuna hatari za kiafya katika jamii.
Machi 12 ilitangazwa kuwa LaLiga itasimama mpaka mwanzoni mwa mwezi April baada ya kikosi cha Real Madrid kulazimishwa kwenda Karantini kufuatia mchezaji mmoja wa kikosi cha Basketball cha Real Madrid kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Lakini sasa maamuzi yamebadilika kutokana na virusi hivyo kuzidi kuathiri nchi ya Hispania zaidi ya watu 2,180 wamefariki mpaka sasa.