VYAKULA WANAVYOPASWA KUTUMIA WACHEZAJI VPL LIGI IKIWA IMESIMAMA
Ligi Kuu Tanzania bara imesimama kwa siku 30 (April 17) hii ni baada ya serikali kuagiza kuwa shughuli zote zinazohusisha mikusanyiko ya watu wengi isimame kwa siku 30.
Baadhi ya wachezaji wa Ligi Kuu Tanzania wameonekana wakijiachia na kurudi makwao kujumuika na famili zao.
Daktari Sufiani Juma ambaye amekuwa akihusika katika tiba michezoni kwa miaka mingi ametoa ushauri kupitia Azam TV wa aina ya vyakula wanavyopaswa kutumia wachezaji ili kulinda utimamu wa miili yao wakati huu Ligi imesimama.
“Kuna vyakula vingi vinavyotumika ambavyo vinapelekea kuhifadhi mafuta ambayo sio mazuri kwa wachezaji, mfano vyakula vya wanga kama vile wali, chapati, maandazi pamoja na ugali na kadhalika vilie lakini kwa kiasi kidogo sana”
”Vyakula vingi vinavyopaswa ni vya protin, vitamini pamoja na mboga mboga, unaweza ukapewa pengine wiki moja inaweza kuwa shida kwa mchezaji kupunguza yale mafuta aliyoyaingiza mwilini kutokana na chakula alichokitumia ndani ya mwezi mmoja”