MEXIME APEWA MKATABA YANGA SC
Kocha wa klabu ya Kagera Sugar ya mjini Bukoba Mecky Mexime ameweka wazi kupitia Azam TV kuwa amepewa mkataba na Yanga SC toka mwishoni mwa mwaka 2019.
Mexime amesema kuwa mkataba huo hajausaini kwa sababu mbili kuna vitu havijakaa sawa lakini pili yeye bado ni muajiriwa wa Kagera Sugar.
“Hilo suala lipo hizi ni kazi nazungumza Yanga kweli walinipa mkataba mpaka sasa hivi ninao ila bado kuna vipengele tu vilikuwa havijakaa sawa, mimi unajua sasa hivi ni muajiriwa naamini mambo yakikaa sawa naamini mimi ni mwalimu nafanya kazi popote”
”Kikubwa kwenye maisha usiangali kuwa mwalimu msaidizi au vipi unaangalia maslahi, mimi naangalia Kagera nakipata kipi na Yanga kama wananitaka watanipa kipi na mimi bado najifunza umri wangu mpaka nije nifikie umri wa kina Mayanga wakina Mkwasa”