NASRI KUJIUNGA NA WEST HAM UNITED
Mchezaji wa zamani wa Arsenal aliyewahi kuichezea Manchester City kwa miaka sita Samir Nasri anatarajia kufanya vipimo vya afya katika klabu ya West Ham United ya nchini Uingereza kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo.
Samir Nasri anatajwa kuwa atajiunga na timu ya West Ham United kwa kipindi hiki akikaribia kumaliza adhabu yake ya kufungiwa miezi 18 kujihusisha na soka, Nasri akifuzu vipimo atasaini mkataba wa miezi minne utakomfanya alipwe Pound 80000 kwa wiki.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa akitumikia adhabu ya kufungiwa miezi 18 kucheza soka kutokana na kubainikia kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni, Nasri akifuzu vipimo hivyo ataungana na kocha wake wa zamani Manuel Pellegrini