BOSS WA OLYMPIACOS NA NOTTINGHAM KAPONA CORONA
Baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona kwa mmiliki wa vilabu vya Olympiacos ya Ugiriki na Nottingham Forest ya nchini England Evangelos Marikanis ,52, sasa amepona.
Mr Evangelos baada ya kuwa chini ya uangalizi (quarantines) kwa wiki mbili amefanyiwa vipimo na kuthibika amepona kabisa virusi hivyo kiasi cha kurejea nyumbani huku akishauri watu waendelee kukaa nyumbani.
Inadaiwa kuwa Mr Evangelos alikutana na kocha wa Arsenal Mikel Arteta siku chache kabla ya kubainika kuwa nae (Arteta) na maambukizi ya virusi vya corona.