SABABU ZILIZOPELEKEA KUCHELEWA KUSOGEZWA MBELE KWA MASHINDANO YA OLYMPIC 2020
Uamuzi wa Kimataifa ya Olympiki (IOC) kutangaza kusogeza mbele mashindano ya Olympic na Paralympic 2020 umechukua muda hata baada ya msukumo toka kwa wanamichezo na nchi washiriki zikiwamo Canada, Australia na Uingereza.
Sababu kubwa zilizopelekea muafaka huu kuchelewa fikiwa zilikuwa sababu za kibiashara na kifedha kwa mashidano haya yenye bajeti ya dola billion 12.6 (takribani shilling trillioni 29 za Kitanzania). Kulingana na IOC hadi sasa zaidi ya zaidi ya “bookings” millioni zimekwisha wekwa kwenye mahoteli mbalimbali ambazo hapna hakika kama nafasi hizi zinaweza patikana tena kama mashindano yatasogezwa mbele.
Kupo na swala la kijiji cha wanamichezo na maeneo mengine muhimu yaliyotengwa yatatumika vipi na kama yataweza pata matumizi mengine baada ya kuwa na makubaliano ya awali na makampuni binafsi swali likiwa kama serikali ya Japan itaweza himili gharama hizo endapo maeneo haya yatabaki wazi bila matumizi mpaka kurejea mashindano haya.
Zaidi kuhairishwa kwa mashindano haya kutaadhiri vyama vingi vya michezo duniani vinavyotegemea mapato ya dola billioni 5 zinazotokana na mashindano haya ambayo sasa yatapelekea sogezwa mbele hadi mwakani.