ETIENNE AELEZA UTARATIBU WAKE TAIFA STARS BAADA YA KUVUNJA KAMBI
Kocha mkuu wa Taifa Stars raia wa Burundi Etienne Ndairagije ametolea ufafanuzi suala la kuvunjwa kwa kambi ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa sababu ya virusi vya corona na mpango wake wa kikosi hicho.
Huku akijibu swali kuwa je mambo yakiwa sawa na ratiba zikapangwa ataita tena kikosi kipya au atatumia kile kile alichokuwa amekiiya kuvunja kambi kwa maagizo ya serikali.
”Timu ya taifa huwa inaitwa kwa muda maalum na mechi maalum kwa kipindi ambacho mmefikia, nikiwa nimeteua wale ni kipindi ambacho cha mechi ya Tunisia tarehe mbayo ilikuwepo, ikiwa watasema kuna mashindano tena tutaangalia tarehe itakuwa ni lini tutaangalia nane anaweza kuwa fiti kwa hilo”