RONADO NA MENDES WATOA BILIONI 2.7 KUSAIDIA MAPAMBANO YA CORONA
Staa wa soka Cristiano Ronaldo na wakala wake Jorge Mendes wametoa msaada wenye thamani ya Pauni milioni 1 (Tsh Bilioni 2.7) katika hospitali nchini Ureno ili kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona
Wawili hao wamekuwa wakifanya mawasiliano na Hospitali hizo ambapo wamepanga kusaidia vifaa katika wodi mbili za Hospitali ya Santa Maria iliyopo Lisbon na wodi moja ya Hospitali ya Santo Antonio mjini Porto
Katika wodi za Santa Maria-Lisbon kila wodi itapewa vitanda 10, ventilator, heart monitors, infusion pumps na syringes na kwa wodi ya Hospitali ya Santa Antonio itapewa vitanda 15, ventilators, Monitors na vifaa vingine.
Imeripotiwa kuwa wodi hizo zitapewa majina yao.
Mpaka sasa nchini Ureno kumeripotiwa kesi 2362 za virusi vya Corona na vifo 29.