GUARDIOLA ARUDI NYUMBANI KUPAMBANA NA CORONA
Janga la virusi vya corona limewafanya watu mbalimbali maarufu kukumbuka kurudisha fadhila nyumbani kwao katika miji na nchi walizotokea.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ametoa msaa wa euro milioni 1 (Tsh Bilioni 2.4) msaada katika jiji la Barcelona ambalo lipo ndani ya Jimbo la Catalonia alilozaliwa kwa ajili ya mapambano ya virusi vya corona.
Msaada huo umetoka ikiwa Hispania Jumanne hii wametoa ripoti kuwa vifo vimefikia 514 ndani ya saa 24, hali ikidaiwa kuwa mbaya zaidi.