MESSI ATOA BILIONI MBILI KUSAIDIA VITA YA CORONA
Staa wa soka Duniani Lionel Messi ametoa msaada wa euro milioni 1 (Tsh Bilioni 2.4) kwa Hospitali kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona.
Msaada huo wa fedha utagawanywa sehemu mbili, kwanza katika Hospital moja jijini Barcelona,Hispania na sehemu nyingine ni Hospitali iliyopo nyumbani kwao Rosario nchini Argentina.
Pia kocha wa zamani wa Lionel Messi, Pep Guardiola ambaye kwa sasa ni kocha wa Man City pia na yeye ametoa msaada wa euro milioni 1 (Tsh Bilioni 2.4) ili kusaidia kupambana na virusi vya Corona katika jiji la Barcelona.
Jana Jumanne nchini Hispania iliripotiwa kufikia vifo 514 katika saa 24 tu, hali ambayo imezidi kuogopesha zaidi.
Takwimu rasmi jana Jumanne zinaonesha nchini Hispania wamefariki jumla ya watu 2,696 mpaka sasa na kesi za waathirika wa virusi hivyo inakaribia 4,000