MECHI ZA KUFUZU AFCON 2021 ZAAHIRISHWA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza kuahirisha Mechi za kufuzu AFCON 2021 zilizokuwa zichezwe kati ya Machi 25 na Machi 31,2020 kwa sababu ya virusi vya Corona.
Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars ilikuwa icheze mechi za kufuzu michuano hiyo dhidi ya Tunisia Machi 27 ugenini na kurudiana nao na Machi 30 jijini Dar es salaam.
Na hivyo sasa hakutakuwa na mechi hizo mpaka pale CAF watakapotangaza vinginevyo.
Mechi nyingine zilizoahirishwa ni za kufuzu kombe la Dunia la wanawake chini ya miaka 20,zilizopangwa kuchezwa Machi 20 mpaka Machi 29,2020 na pia mechi za kufuzu michuano ya AFCON ya wanawake 2020 iliyopangwa kuchezwa April 8 mpaka April 14 mwaka huu.