CORONA YASIMAMISHA LIGI YA ITALIA
Mechi nne za Serie A ziliahirishwa jana Februari 23 kwa hofu ya mlipuko wa Corona Virus nchini Italia ambapo watu wawili walioathirika na virusi hivvyo wamefariki dunia nchini humo.
Kwa agizo la serikali ya Italia, mechi hizo zilizoahirishwa ni Atalanta vs Sassuolo, Hellas Verona vs Cagliari,Torino vs Parma na Inter Milan vs Sampdoria.
Mechi hizo zilizoahirishwa ni za mikoa ya kaskazini mwa nchi ya Italia——ambapo ndipo kumetajwa kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huo.
Katika siku ya Jumamosi zaidi ya mechi 40 za mtaani na za vijana katika mikoa hiyo ziliahirishwa kwa sababu ya hofu ya virusi vya Corona.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Italia, mechi ya nyumbani ya Inter Milan ya raundi ya 32 bora Europa League dhidi ya Ludogorets kutoka Bulgaria, ipo mashakani pia kuchezwa