Dani Alves kutua ligi kuu nchini England
Kabla hajamaliza maisha ya kucheza soka ni lazima acheze katika ligi kuu nchini England, amesema beki wa klabu ya PSG Dani Alves.
Beki huyo,35, ambaye anakaribia kurejea dimbani tangu aumie goti lake mwezi Mei mwaka huu, ameyasema matamanio yake ya kucheza katika ligi kuu nchini England.
“ Wazo la kwamba nitamaliza maisha yangu ya soka bila kwenda kucheza Premier halipo “ ameuambia mtandao wa Telegraph.
‘ Kwa kweli , (Premier League) ni moja ya soka la maajabu duniani. Kwanza, kwa sababu ya heshima kwa wachezaji kutoka kwa mashabiki , na pia sababu ya shauku iliyopo uwanjani ‘
Alves ambaye ameshinda makombe 38 kwenye maisha yake ya soka, alikataa ofa ya kujiunga na Man City mwaka 2017 wakati akijiunga na PSG akitokea Juventus.