RAIS WA CAF KUHUDHURIA MECHI YA WATANI WA JADI
Rais wa shirikisho la soka la Afrika CAF Ahmad Ahmad anataraji kuwasili nchini Tanzania Machi 7 kwa ziara yake ya siku tatu kwa mwaliko wa TFF.
Katika Ziara hiyo Ahmad Ahmad atahudhuria mechi ya watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba itakayopigwa Jumapili Machi 08 Uwanja wa Taifa Dsm.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Ahmad Ahmad kuhudhiria mechi ya Watani wa Jadi tangu achuguliwe kuwa Rais wa CAF Machi 16,2017.
Ahmad Ahmad,60, ambaye ni raia wa Madagascar, ni Rais wa saba wa shikikisho hilo la soka barani Afrika CAF.