MORRISON AWALAZA NJAA SIMBA
Ni Bernard Morrison ndiye aliyepelekea shangwe mitaa ya jangwani na huzuni kutawala Msimbazi.
Goli lake la mpira wa adhabu dakika ya 44 dhidi ya kipa Aishi Manula ndilo lililodumu mpaka filimbi ya mwisho ya Martin Saanya kutoka Morogoro.
Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu baada ya ule wa mzunguko wa kwanza kuisha kwa sare ya 2-2,Yanga akitokea nyuma kwa goli 2-0 na kusawazisha