MISRI WASIMAMISHA MASHINDANO YOTE
Chama cha soka nchini Misri (EFA) kimetangaza kusitisha mashindano yote ya soka kwa sababu ya mlipuko wa virusi vya corona ambavyo vimeingia nchini kwao.
Hadi sasa ni zaidi ya watu 55 wameripotiwa Misri kupata maambukizi ya virusi vya corona, hali ambayo imeilazimu serikali kuamuru kufungwa kwa shule na vyuo vikuu kama sehemu ya kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.