RAIS WA GHANA ASIMAMISHA MICHEZO
Rais wa taifa la Ghana Nana Addo ametangaza kuwa shughuli zote za kimichezo nchini humo zisimamishwe kwa muda wa wiki nne ili kupisha kuenea kwa virusi corona.
Tangaza hili lililototelewa na Rais Nana jijini Accra nchini Ghana Jumapili ya Machi 15 2020, kama hatua za awali za kupunguza na kuondoa mikusanyiko ambaye ingeweza kusababisha maambukizi kuenea.
Hadi sasa nchini Ghana idadi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona na kuthibitika inadaiwa kufikia sita baada ya jana wizara ya afya ya nchini humo kutangaza wanne.