DERBY YA SIMBA NA YANGA YAANDIKA HISTORIA SERIKALINI
Serikali ya Tanzania kupitia kwa msemaji mkuu wa serikali Dr Hassan Abbas ametangaza kuwa mchezo wa Simba na Yanga uliyochezwa Machi 8 uwanja wa Taifa kuingiza mapato makubwa kwa serikali ambayo haijawahi kutokea.
“Mchezo wa Simba na Yanga uliochezwa Machi 8, 2020 umeweka rekodi ya mapato kwa kuingiza shillingi Milioni 545.4 kwa timu na mapato ya Serikali shillingi Milioni 153.2 ambayo hayajawahi kupatikana wakati wote katika historia ya Simba na Yanga” alisema Dr Hassan Abbasi kwenye mkutano na waandishi
Tukukumbushe tu mchezo wa watani wa jadi wa Simba na Yanga uliyochezwa Machi 8 2020 uwanja wa Taifa uliingija jumla ya watazamaji 59,325, mapato yakiwa zaidi ya Tah milioni 545, uwanja ukiwa na uwezo wa kuchukua watu 60,000.