ALAN SHEARER AWAPOKONYA UBINGWA LIVERPOOL
Alan Shearer amesema kuwa Liverpool hawawezi kupewa ubingwa kama msimu huu wa ligi kuu nchini England hautokamilika kwa sababu ya virusi vya Corona.
Liverpool mpaka msimu unasimamishwa, wapo juu kwa pointi 25 na wanahitaji ushindi wa mechi mbili tu kuchukua ubingwa huo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 30.
Ligi hiyo sasa imesimamishwa mpaka April 3 katika kipindi hicho cha janga la virusi vya Corona.
Mpak sasa hakuna uhakika kama msimu huu wa ligi kuu utaendelea baada ya tarehe hiyo, wengine wakihofia huenda ukafutwa kabisa.
“Kama, msimu hautoweza kukamilika basi hakuna namna unaweza kuwa na mshindi au mshindwa.” Aliandika Shearer katika makala yake ya gazeti la TheSun.
“Kama hauwezi kukamilisha michezo basi hauwezi kutoa ubingwa au kumshusha daraja yoyote”
“Kwa Liverpool, itakuwa ni ngumu sana”
“Wanahitaji pointi sita tu lakini bado hawajazipata, kwa hiyo kwa sababu hiyo inatakiwa kutangazwa ni batili na tupu”