LIGI KUU TANZANIA BARA YASIMAMA KWA SABABU YA CORONA
Serikali ya Tanzania kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa imetangaza kusimamisha Ligi Kuu Tanzania Bara,Ligi Daraja la Kwanza na la Pili,UMITASHUMTA na UMISETA na ile ya Mashirika ya Umma kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kujilinda na virusi vya Corona.
Virusi vya Corona ambavyo vimekuwa vikisambaa nchini mpaka nchi, vimetangazwa kuingia nchini Tanzania baada ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu jana kuthibitisha Raia wa Tanzania Mwanamke mwenye umri wa miaka 46 kukutwa muathirika wa virusi hivyo.
Mwanamke huyo aliwasili nchini Tanzania kutoka Ubelgiji kupitia uwanja wa KIA.
Mpaka sasa Ligi Kuu Tanzania Bara baadhi ya timu zimecheza mechi 28,29,na nyingine 27. Simba wakiwa kileleni kwa Jumla ya Pointi 71,huku Singida United wakishika mkia kwa kukusanya pointi 15.