MANE AIKUMBUKA NCHI YAKE JANGA LA CORONA
Mshambuliaji nyota wa Liverpool na timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane ameonesha kuguswa na taifa lake la Senegal wakati huu wa mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona.
Mane ameamua kuichangia nchi yake kiasi cha euro 45,000 (Tsh milioni 125) kama sehemu ya kuwezesha serikali yake kupambana na maambukizi ya virusi vya corona ambapo Senegal ni miongoni mwa nchi zilizo athirika.
Hadi kufikia Machi 14 kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari viliripoti kuwa Senegal kuna wagonjwa 22 waliokuwa chini ya uangalizi kwa virusi vya corona na wawili kati yao kudaiwa kutoroka.