FLOYD MAYWEATHER APATA PIGO
Bondia wa kimarekani Floyd Mayweather amepata pigo baada ya mtandao wa TMZ kuripoti taarifa kuwa amefiwa na mjomba wale Roger Mayweather.
Roger Mayweather ,58, alikuwa hayupo na afya njema na alikuwa pia akisumbuliwa na kisukari, Roger alikuwa sehemu ya makocha wa Floyd Mayweather waliomtengeneza kuwa bondi bora duniani, hata hivyo marehemu Roger ashawahi kuwa Bingwa wa boxing
Floyd anakuwa kapata pigo la kupoteza watu wake wawili muhimu ndani ya wiki moja baada ya wiki iliyopita kuripotiwa kifo cha Josia Harris ambaye ni mama wa watoto wake na sasa mjomba wake Roger aliyestaafu ngumi 1999.