BANDA ATHIBITISHA KUHUSU CORONA
Beki wa kati wa klabu ya Highlands Park ya nchini Afrika Kusini Abdi Banda amekanusha taarifa za kupata maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).
Taarifa hizo Banda ametoa kupitia ukurasa wake wa instagram ikiwa ni siku moja imepita toka zisambae taarifa za kuwa anaugua corona.
“Napenda kutoa shukrani zangu kwa wote mlioguswa/shtushwa na habari juu yangu kikubwa kila kitu kimeenda sawa na kwa baraka za M/MUNGU imegundulika haukuwa ugonjwa unaosumbua kwa sasa duniani👏. Ahsanteni sana MUNGU awabariki” >>> Abdi Banda